MapService
Huduma na bei Layout Inavyofanya kazi Kuhusu sisi Maswali Tafuta oda yangu
Kiswahili · English Tengeneza ramani
Huduma na bei Layout Inavyofanya kazi Kuhusu sisi Maswali Tafuta oda yangu Piga +255 759 001 714 English

Faragha na masharti ya majaribio

Rasimu ya tarehe 13-11-2026. Huduma hii iko katika majaribio (beta).

Majaribio (beta)

  • Wakati wa majaribio, ramani, QGIS project na mabadiliko ni bure.
  • Huduma inaweza kusimama kwa muda au kubadilika bila taarifa. Tunajitahidi, lakini hatuahidi kuwa itapatikana muda wote.
  • Ramani ni za taarifa: zinatumia mipaka ya kata ya Sensa ya 2022 (NBS), OpenStreetMap na data ya satelaiti, ambazo zinaweza kuwa na mapungufu. Hakiki na vyanzo rasmi kabla ya kuzitumia kwa usanifu, mipaka ya ardhi au jambo la kisheria.
  • Tuma tu data uliyo na ruhusa ya kuitumia. Usitume taarifa za siri usizohitaji kwa ramani.
  • Tunaweza kutumia maoni yako (bila jina lako) kuboresha huduma.

Tunachokusanya

  • Mahali pa mradi: ulichochora, faili uliyotuma, au kata uliyochagua.
  • Jina la mradi na maelezo ya ramani uliyoandika (mteja, mshauri, anwani, nembo).
  • Email au namba ya simu, ili tukutumie link na uweze kuipata ramani tena.
  • Maoni, faili na voice note unaotuma kwa mabadiliko.
  • Kumbukumbu za kiufundi (kurasa zilizofunguliwa na muda), cookie moja ya lugha uliyochagua, na cookie yenye namba ya bahati nasibu inayotusaidia kuhesabu wageni na hatua walizofikia. Haina jina lako, anwani ya mtandao wala barua pepe.

Tunavyotumia

Kutengeneza ramani yako, kuwasiliana nawe kuhusu oda hiyo, na kuboresha huduma. Hatuuzi taarifa zako wala hatutumi matangazo. Tunakuandikia kwa WhatsApp tu ukiruhusu.

Muda tunaohifadhi

Faili zako na ramani zinafutwa siku 30 baada ya shughuli ya mwisho ya oda. Kumbukumbu fupi ya oda (namba, mawasiliano, tarehe) inabaki kwa hesabu.

Zinapohifadhiwa

Wakati wa majaribio, data inahifadhiwa kwenye kompyuta yetu hapa Tanzania. Mawasiliano kati ya simu yako na tovuti yanapita kwa Cloudflare, kampuni ya kimataifa inayolinda na kusafirisha mtandao.

Haki zako

Unaweza kuomba kuona, kusahihisha au kufuta taarifa zako wakati wowote: tuandikie kwa WhatsApp au piga +255 759 001 714, ukitaja namba ya oda.

Hii ni rasimu kwa kipindi cha majaribio. Itakaguliwa kisheria kabla huduma haijaanza kutoza.

MapService

Ramani za Tanzania kwa ripoti, maandiko ya miradi na zabuni. Papo hapo kutoka kwenye mfumo, na tunazirekebisha sisi wenyewe unapohitaji mtu.

Huduma

  • Ramani ya papo hapo
  • Mabadiliko kwenye ramani yako
  • Ramani maalum
  • Tafuta oda yangu
  • Faragha na masharti ya majaribio

Faili zako

Zinahifadhiwa siku 30 baada ya shughuli ya mwisho ya oda yako. Link ya oda yako ni ya siri: yeyote mwenye link hiyo anaweza kuiona oda.

Mawasiliano

  • +255 759 001 714
  • WhatsApp
  • Jumatatu-Ijumaa 08:00-17:00 · Jumamosi-Jumapili 09:00-15:00
Boundaries: NBS 2022 Population and Housing Census · Natural Earth · Elevation: Copernicus DEM · Background maps © OpenStreetMap contributors (ODbL)