Ramani za Tanzania

Ramani yako kwa dakika moja. Marekebisho na mtaalamu ndani ya saa chache.

Tuonyeshe mradi wako ulipo upate ramani ya mahali ilipo, tayari kwa ripoti, yenye ramani ndogo za nchi, mkoa, wilaya na kata. Iangalie bure kwanza, lipa kwa simu, pakua PDF.

Iangalie kabla ya kulipa M-Pesa · Mixx · Airtel · HaloPesa Unahudumiwa na mtaalamu wa ramani, si mashine
Mfano wa ramani ya mahali mradi ulipo
FIG. 01 · PROJECT LOCATION MAP · CLASSICA3 · UTM 37S
Inavyofanya kazi

Hatua nne. Huhitaji programu wala akaunti.

  1. 01

    Tuonyeshe mahali

    Tafuta mahali na gusa ramani, chora mstari au eneo, au tuma faili ya GIS.

  2. 02

    Ipe jina

    Andika jina la mradi na email au simu yako, uweze kuipata ramani tena.

  3. 03

    Ona preview ya bure

    Ona karatasi nzima. Badilisha mwonekano mara nyingi upendavyo.

  4. 04

    Lipa na pakua

    Lipa kwa simu. PDF na PNG zinatengenezwa mara tu malipo yakithibitishwa.

Tengeneza ramani yangu: preview ya bure
Mifano ya ramani

Layout tano, ubora ule ule.

Data ile ile, usahihi ule ule. Chagua layout inayofaa ripoti, andiko au zabuni yako. Unaweza kubadilisha bure kwenye ukurasa wa preview.

Classic engineering

Classic engineering

Classic · insets right

Classic · insets right

Classic · title strip

Classic · title strip

Classic · no title block

Classic · no title block

Classic · print-friendly

Classic · print-friendly

Classic · serif

Classic · serif

Kilichopo kwenye kila karatasi Ramani ndogoMshale wa kaskaziniScale barGrid LegendTitle blockBarabara na majina ya maeneo Land coverContours
Huduma na bei

Anza papo hapo. Mtaalamu yupo ukimhitaji.

Chagua ramani unayotaka

Kuanzia papo hapo hadi kazi ya mtaalamu

  • Muda ulioahidiwa kwa kila ombi. Unauona kabla hatujaanza.
  • Preview ya bure, bei maalum. Hakuna mshangao baada ya kulipa.
  • Ongea ukipenda. Piga simu, WhatsApp, au tuma voice note, kwa Kiswahili au Kiingereza.
Maswali

Maswali ya mara kwa mara

Sina faili ya GIS. Bado naweza kupata ramani?

Ndiyo. Tafuta kijiji, kata au shule, kisha gusa ramani mahali mradi ulipo. Unaweza pia kuchora mstari (barabara au bomba) au eneo (kiwanja au skimu).

Naweza kutuma faili za aina gani?

Shapefile iliyo kwenye zip, KML au KMZ, GeoJSON, GeoPackage, DXF, au CSV yenye coordinates (hadi MB 50).

Nalipaje?

Baada ya preview ya bure, andika namba yako ya M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa na uthibitishe malipo kwenye simu kwa PIN. Ukurasa unathibitisha wenyewe na ramani yako inatengenezwa papo hapo. Unaweza pia kulipa kwa namba yetu ya Lipa na kuandika namba ya muamala.

Nimepoteza link ya ramani yangu. Nifanye nini?

Fungua Tafuta oda yangu na uandike namba ya oda pamoja na email au simu uliyotupa.

Faili yangu haina mfumo wa coordinates. Itafanya kazi?

Ndiyo. Tunajaribu mifumo ya kawaida ya Tanzania (WGS 84, Arc 1960, UTM) na kukuonyesha orodha fupi ya mahali inapoweza kuwa. Unabofya mahali sahihi.

“Saa 3-6 za kazi” inamaanisha nini usiku au mwisho wa wiki?

Muda unahesabiwa wakati wa saa za kazi tu (Jumatatu-Ijumaa 08:00-17:00, Jumamosi-Jumapili 09:00-15:00). Marekebisho madogo yakitumwa saa 10 jioni siku ya kazi yanapata saa moja siku hiyo na yanakuwa tayari saa 4 asubuhi inayofuata.

Faili zangu zinahifadhiwa kwa muda gani?

Zinahifadhiwa siku 30 baada ya shughuli ya mwisho ya oda yako. Link ya oda yako ni ya siri: yeyote mwenye link hiyo anaweza kuiona oda.

Unapendelea kuongea kuliko kuandika?

Wasiliana nasi moja kwa moja.

Tunajibu wakati wa saa za kazi. Voice note kwa Kiswahili au Kiingereza unakubalika.
Jumatatu - Ijumaa 08:00-17:00 · Jumamosi - Jumapili 09:00-15:00